Eterniseed

Zaburi 13

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu · Kiswahili · Free, openly licensed

1 Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako hadi lini?

2 Nitapambana na mawazo yangu hadi lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda hadi lini?

3 Nitazame, unijibu, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.

4 Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

5 Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

6 Nitamwimbia Mwenyezi Mungu, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Read Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu with narration, notes, and lessons in the Eterniseed app.