1 Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!
2 Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Haruni, hadi kwenye upindo wa mavazi yake.
3 Ni kama umande wa Hermoni ukianguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake, naam, uzima hata milele.
Read Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu with narration, notes, and lessons in the Eterniseed app.